SayansiAsia
India yatuma chombo kulifanyia utafiti Jua
2 Septemba 2023Matangazo
Roketi iliyobeba chombo hicho cha utafiti wa Jua kilichopewa jina la Aditya-L1, iliruka mapema leo alfajiri kuanza safari ya kiasi umbali wa kilometa milioni 1.5 kutoka sayari ya dunia.
Shirika la Utafiti wa Anga za Juu la India limesema chombo hicho kitatafiti tabaka la juu la Jua, maumbile na upepo kwenye nyota hiyo yenye dhima kuu katika mfumo wa sayari unaoijumuisha dunia.
Hatua hiyo inafuatia mafanikio ya mnamo Agosti 23 ambapo India ilikuwa taifa la kwanza duniani kupeleka chombo kwenye ncha ya kusini mwa mwezi. Utafiti kuhusu Jua na mafanikio ya kutuma chombo mwezini kunaimarisha nafasi ya India katika shughuli za utafiti wa anga za juu duniani.