Infantino kugombea bila kupingwa kuwa rais wa FIFA
6 Februari 2019Infantino mwenye umri wa miaka 48 amekuwa akiendesha shirikisho hilo la FIFA tangu Februari mwaka 2016.
wakati huo huo rais wa shirikisho la kandanda nchini Ujerumani DFB , Reihard Grindel ametoa wito kwa rais wa FIFA Gianni Infantino kuweka mahusiano na shirikisho la kandanda barani Ulaya kuwa mazuri muda mfupi kabla ya kuchaguliwa tena katika baraza la shirikisho hilo la kandanda duniani.
"Nitakuwa na furaha kubwa iwapo tutakuja pamoja katika ushirikiano wenye maana kati ya FIFA na UEFA. Hii hata hivyo inahitaji uwazi na tafakuri katika maslahi ya Ulaya kutoka upande wa FIFA," Grindel ameliambia shirika la habari la dpa kabla ya mkutano wa kamati ya utendaji ya UEFA mjini Rome siku ya Jumatano(06.02.2019).
Grindel anagombea bila kupingwa ili kuchaguliwa tena kuingia katika baraza la FIFA na hakutoa ahadi, hata kama kulikuwa na mzozo kati ya vyombo hivyo vya Ulaya na dunia kwa muda sasa.