Iran ibadili utaratibu wake au itakabiliwa na vikwazo zaidi
13 Novemba 2007LONDON: Iran ibadili
Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown ameahidi kuhimiza vikwazo vikali zaidi kuwekwa dhidi ya viwanda vya mafuta na gesi vya Iran.Akizungumza kwenye dhifa ya kila mwaka ya Meya wa Jiji la London,Brown aliionya Tehran kuwa hatua hiyo itachukuliwa kama ripoti inayongojewa kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran haitoonyesha maendeleo.
Amesema,Iran ina chaguo:ama mpambano na jumuiya ya kimataifa na hivyo kusababisha vikwazo kuimarishwa au uhusiano mpya na ulimwengu,ikiwa itabadilisha utaratibu wake na kuacha kuunga mkono ugaidi.
Hotuba ya Brown hasa ilihusika na sera za nje na akasisitiza uhusiano wa karibu uliopo kati ya Uingereza na Marekani.Akaongezea kuwa amefurahi kuona Ujerumani na Ufaransa zikikaribiana na Marekani,baada ya mivutano iliyozuka mwanzoni mwa vita vya Irak mwaka 2003.