Iran kufanya mazungumzo na mataifa ya Ulaya kuhusu nyuklia
2 Januari 2025Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Iran Kazem Gharibabadi ameeleza kuwa duru mpya ya mazungumzo kati ya Iran na mataifa matatu ya Ulaya yenye nguvu yatafanyika mjini Geneva, japo ameongeza kuwa, yatakuwa ni "mashauriano tu na wala sio majadiliano."
Nchi hizo tatu za Ulaya zimeituhumu Iran kwa kuongeza hifadhi yake ya madini ya Urani iliyorutubishwa kwa kiwango cha kutisha bila ya kuwepo sababu yoyote ya wazi ya matumizi ya ndani.
Soma pia: Iran yairuhusu IAEA kuongeza ukaguzi wa nyuklia
Nchi hizo pia zimeeleza uwezekano wa kurejesha vikwazo dhidi ya Iran ili kuizuia Jamhuri hiyo ya Kiislamu kuendeleza mpango wake wa nyuklia.
Mwanadiplomasia mkuu wa Iran Abbas Araghchi amesema nchi yake iko tayari kufanya mazungumzo "kwa njia ya haki na yenye heshima” na mataifa ya Magharibi.