Iran yakiri kufanya mashambulizi Iraq
14 Machi 2022Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, Mshauri wa Kitaifa katika masuala ya Kiusalama wa Marekani Jake Sullivan amesema wataiunga mkono serikali ya Iraq katika kuiwajibisha Iran, na kadhalika kuwaunga mkono washirika katika kanda yote ya Mashariki ya Kati katika kukabiliana vitisho vyenye kufanana na hivyo kutoka Iran.
Iran yadai kuhusika na shambulizi
Iran imedai kuhusika na shambulizi la kombora karibu, karibu na ubalozi mdogo wa Marekani huko mjini Erbil, mji mkuu wa eneo lenye mamlaka ya kadri la Kurdistan.
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi cha Iran (IRGC) kimedai kambi ya kijasusi ya Waisrael ndio ilikuwa wakiilenga. Na lilikuwa pia shambulizi la kulipiza kisasi kutokana yale yanayohisiwa mashambulizi ya Israel ya Damascus, Syria ya juma lililopita ambayo yaliwauwa Wairan wawili.
Iran imeongeza kusema inasema eneo hilo lilikuwa la kimkakati kivita ingawa mamlaka ya Kikurd katika eneo hilo ilisisitiza kwamba Israel, taifa la Kiyahudi halina eneo lolote linalowahusu ndani ya Arbil au hata karibu na mji huo.
Iraq yalalamika kuingiliwa mamlaka yake.
Wizara ya mambo ya nje ya Iraq imemwita balozi wa Iran nchini, Iraj Masjidi humo kwa lengo la kupinga shambulizi hilo. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP, hatua hiyo pamoja na mengineyo ina lengo la kulaani, kile kinachoelezwa ukiukwaji mkubwa wa mamalaka ya Iraq.
Shambulizi hilo, limesababisha hasahara katika maeneo kadhaa ikiwemo ya maeneo ya viwanda na makazi ya watu wa kawaida. Mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP, anasema alisikia mivumo mitatu ya makombora kabla hakujakuchwa Jumapili.
Dereva wa teksi Ziryan Wazri anasema alikuwa katika gari yake wakati sauti za makombora hayo ziliposikika. Anasema zilikuwa sauti kali, zilizoambatana na moshi mzito hewani. Lakini pia yeye hakunusurika kwa kuwa vishindo vilivunja vioo vya gari yake nae pia akajeruhiwa usoni.
Iran inatazamwa kama taifa lenye kuwa na ushawishi kwa serikali ya Iraq, na Iraq kadhalika bado ina wanajeshi kadhaa wa Marekani, ambao wanashiriki operesheni maalumu dhidi ya Kundi la Dola la Kiislamu.
Chanzo: RTR/AFP