1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yamnyonga Jamshid Sharmahd raia wa Ujerumani na Iran

29 Oktoba 2024

Wabunge wa Ujerumani wamelaani kunyongwa nchini Iran kwa Jamshid Sharmahd mwenye uraia wa Iran na Ujerumani kwa mashitaka ya ugaidi na kuonya kuhusu madhara ya kidiplomasia.

https://p.dw.com/p/4mKXr
Iran | Jamshid Sharmahd
Jamshid Sharmahd inaaminika alitekwa na vikosi vya Iran mjini Dubai mwaka wa 2020Picha: Koosha Falahi/Mizan/dpa/picture alliance

Sharmahd alinyongwa Jumatatu asubuhi, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya idara ya mahakama ya Iran Misan. Serikali ya Ujerumani ilikuwa imekosoa vikali hukumu yake na kwa muda mrefu ilitaka Sharmahd aachiliwe huru.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amelaani vikali utekelezwaji wa hukumu hiyo ya kifo, akisema Ujerumani iliituma mara kadhaa nchini Iran timu ya ngazi ya juu.

Kiongozi wa chama cha Kihafidhina nchini Ujerumani cha Christian Democratic Friedrich Merz alilaani adhabu hiyo ya kunyongwa akisema ni "uhalifu mbaya mno". Alitoa wito wa kufukzwa balozi wa Ujerumani mjini Berlin.

Soma pia: Ujerumani yakosoa hukumu ya kifo kwa raia wake, Iran

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki za Binaadamu na Misaada ya Kiutu Renata Alt aliita hukumu hiyo "habari za kutisha" na kusema ni uthibitisho zaidi kuwa hakuna mazungumzo yoyote yanayowezekana kufanywa na utawala wa kigaidi."