Iran yasema itajadiliana na IAEA ila haitokubali shinikizo
14 Novemba 2024Haya yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Abbas Araqchi, katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, baada ya mkutano wake na mkuu wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa, Rafael Grossi.
Grossi afanya ziara Iran kwa ajili ya "suluhu la kidiplomasia"
Kwa upande wake mkuu wa nyuklia wa Iran Mohammad Eslami amesema kuwa mkutano wake na Grossi umekwenda vizuri ila akadai kuwa Iran itajibu mara moja azimio lolote dhidi yake katika mkutano na IAEA wiki ijayo, bila kutoa maelezo zaidi.
Wanadiplomasia wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba nchi zenye nguvu Ulaya zinalitaka shirika hilo la nishati ya Atomiki kuiwekea Iran azimio jipya katika huo mkutano wa wiki ijayo ili kuishinikiza Tehran, kutokana na kile wanachosema ni ushirikiano wake duni.