1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UgaidiIran

Iran: Washukiwa 3 waliokuwa wakipanga mashambulizi wakamatwa

6 Aprili 2024

Polisi nchini Iran imewakamata washukiwa watatu wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu waliokuwa wakipanga mashambulizi mwishoni mwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, vyombo vya habari vimeripoti siku ya Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4eUjC
Washukiwa wa mashambulizi wakiwasilishwa mjini Teheran
Washukiwa wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS waliokamatwa nchini IranPicha: Fars

Washukiwa hao waolikamatwa katika mji wa Karaj, katika jimbo la kaskazini magharibi la Alborz, ni Mohammed Zakar anayetambuliwa kama afisa mwandamizi wa kundi hilo, hii ikiwa ni kulingana na  shirika la habari la Iran, IRNA.

Hata hivyo, shirika hilo halikuweka wazi mara moja, ni wapi washukiwa hao walikamatwa au kama kulikuwa na raia wa kigeni.

IRNA pia liliripoti juu ya kukamatwa kwa watu wengine wanane waliohusishwa na mpango huo, lakini hakukuwa na maelezo zaidi.

Mwezi Januari, IS walitangaza kuhusiaka na mashambulizi mawili katika jiji la kusini mwa Iran la Kerman, yaliyowaua zaidi ya watu 90.