1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq na Umoja wa Mataifa wakumbuka shambulio la 2003

Sylvia Mwehozi
19 Agosti 2023

Maafisa wa Iraq na Umoja wa Mataifa, leo wamefanya kumbukumbu ya miaka 20 ya shambulio baya la kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Baghdad.

https://p.dw.com/p/4VM2Q
Bango la picha ya Saddam Hussein
Gari ya UN ikilipita bango la aliyewahi kuwa kiongozi wa Iraq Saddam Hussein Picha: Ahmad Al-Rubaye/dpa/picture-alliance

Maafisa wa Iraq na Umoja wa Mataifa, leo wamefanya kumbukumbu ya miaka 20 ya shambulio baya la kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Baghdad.

Shambulio la Agosti 19 mwaka 2003 katika jengo la Umoja wa Mataifa mjini humo liliwaua watu 22, na linatajwa kuwa shambulio baya dhidi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika historia.JE UMOJA WA MATAIFA UTAREJEA IRAQ:

Lilitokea katikati mwa uvamizi ulioongozwa na Marekani nchini Iraq na kumwondoa kiongozi wa kidikteta Saddam Hussein, lakini likachochea uasi na miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi katika taifa hilo.

Mkuu wa ujumbe wa usaidizi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Jeanine Hennis-Plasschaert, amesema wakati wa kumbukumbu ya leo kwamba majeraha yaliyotokana na shambulio hilo na vurugu zilizojitokeza baadae, hayawezi kupona kikamilifu.