Iraq yalaani mashambulizi ya Iran
16 Januari 2024Matangazo
Wizara ya mambo ya nje kupitia taarifa imeeleza kuwa mamlaka ya Iraq itachukua hatua zote za kisheria zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Pia watachapisha matokeo ya uchunguzi juu ya mashambulizi hayo, ili kuuthibitishia umma wa kimataifa juu ya madai ya uwongo yanayotolewa na wale waliohusika na vitendo hivyo.
Taarifa ya Iraq imetolewa baada ya jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran kusema kwamba lilishambulia "makao makuu ya kijasusi ya Israel" huko Kurdistan.
Mashambulizi hayo yanatokea katikati ya wasiwasi wa kuongezeka kwa mizozo eneo la Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas.