1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIreland

Ireland kumpata waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi

25 Machi 2024

Ireland iko tayari kumpata waziri mkuu wake mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea mwezi ujao baada ya Simon Harris kupata uongozi wa chama cha Fine Gael, akichukua nafasi ya Leo Varadkar aliyetangaza kujiuzulu

https://p.dw.com/p/4e4v0
Simon Harris, achaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Fine Gael
Simon Harris atakuwa waziri mkuu wa Ireland mwenye umri mdogo zaidiPicha: Eamon Ward/AP Photo/picture alliance

Harris mwenye umri wa miaka 37, aliyekuwa waziri wa elimu ya juu wa serikali ya mseto, alikuwa mgombea pekee kuwasilisha jina lake kumrithi Varadkar aliyejiuzulu wiki iliyopitana ambaye awali alikuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo nchini Ireland.

Harris anatarajiwa kuchaguliwa rasmi kuwa waziri mkuu katika bunge la Ireland mapema Aprili baada ya wabunge kurejea kutoka likizo yao ya Pasaka. Katika hotuba yake ya ushindi jana, Harris alisema huu ni wakati wa chama cha Fine Gael kuungana tena na watu na akaahidi kupambana dhidi ya nguvu za siasa kali za kizalendo katika siasa za Ireland.

Alithibisha kuwa chama cha Fine Gael kinajivunia kuunga mkono sera za Ulaya, akalaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na kutoa wito wa kusitishwa maramoja kwa mapigano huko Gaza kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.