SiasaSyria
IS yathibitisha kifo cha kiongozi wake huko Syria
4 Agosti 2023Matangazo
Kundi hilo lilisema kwamba kiongozi wake aliuawa katika mapigano ya moja kwa moja na kundi jingine katika mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria unaodhibitiwa na waasi.
Soma pia: Kundi la IS latangaza kifo cha kiongozi wake
Hii ni mara ya kwanza kwa IS kutoa tamko rasmi tangu Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki aliposema mwezi Aprili kuwa idara zake za kijasusi zilimuua kiongozi huyo nchini Syria.
Erdogan alidai kuwa idara ya usalama wa taifa ya Uturuki ilikuwa ikimsaka Quraishi kwa muda mrefu. Wanamgambo wa IS wanaendelea kufanya mashambulizi ya waasi nchini Syria na Iraq.
Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani pamoja na ule unaoongozwa na Wakurdi bado pia unaendelea kupambana na mashambulizi ya IS nchini Syria.