1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel haikujiandaa kwa vita vya Gaza 2014

Admin.WagnerD1 Machi 2017

Taasisi ya uchunguzi nchini Israel imemtuhumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na maafisia wa jeshi kwa kutojiandaa vyema na kitisho cha kimkakati kilichotokana na matumizi ya mahandaki katika vita vya Gaza vya mwaka 2014

https://p.dw.com/p/2YQnf
Gaza: Israelische Kampfflugzeuge Bombe
Moja kati ya matukio ya vita vya Gaza vilivyodumu kwa siku 50 mwaka 2014Picha: picture alliance/Pacific Press/N. Alwaheidi

Matokeo ya uchunguzi huo uliofanyika katika kipindi cha miaka miwili yamesababisha tafrani katika mwenendo wa siasa za Israel, ambapo wakosoaji wa Netanyahu wanatumia fursa hiyo kumesema waziri mkuu huyo anaedaiwa kuingilia kiujanja mchakato wa utowaji maamuzi. Mdhibiti wa taifa,Yossef Shapira amesema katika ripoti huiyo  kuwa wadau muhimu kwa upande wa kisiasa, kijeshi na kijajsusi ulikuwa na taarifa juu ya kitisho cha mahandaki na hata kuelezwa kama mkakati.

Afisa huyo mwandamizi aliongeza kusema pamoja na yote hayo lakini hatua zilizochukuliwa katika kushughulikia kitisho hicho hazikulingana na namna tatizo halisi lilivyoainishwa. Kimsingi ripoti inasema Netanyahu na baadae waziri wa ulinzi Moshe Yaalon hawakupeana taarifa kwa ukamilifu walizokuwa nazo kuhusu mahandaki pamoja na wajumbe wengine katika baraza la usalama badala yake waliziwasilishwa kwa ufinyu na namna ya kawaida tu.

Baraza la mawaziri halikuwa na taarifa za kina

Washington Israle Min isterpräsident Netanjahu bei Pk mit Trump
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin NetanyahuPicha: picture-alliance/newscom/P. Benic

Ripoti hiyo vile vile inasema wawili hao walishindwa kuwapa mawaziri habari muhimu na za kina zitakazowazesha kufanya uamuzi mzuri kuhusu hali ya mambo katika eneo la gaza kabla ya Israel kujiingiza katika vita. Lakini baada ya kutolewa ripoti hiyo kwa mara nyingine Netanyahu aliikingia kifua rekodi yake, kwa kusema kitisho cha mahandaki kimejadiliwa katika baraza la mawaziri mara 13.

Alisema vita hivyo vilikuwa na mafanikio ambapo Israel ilikabiliana na ukatili wa kundi la Hamas tangu kuanza kwake. Aliongeza kusema Israel imewaua magaidi takribani 1,000 na kuangamiza maelfu ya maroketi.

Malengo muhimu ya Israel katika awamu ya tatu ya operesheni yake ya kijeshi kwenye eneo la pwani katika kipindi cha miaka sita ni kuyaharibu maandaki na kukifikisha kikomo vitendo vya wanamgambo wa Kipalestina katika eneo la Gaza, na hasa Hamas kuishambulia kwa maroketi katika ardhi ya Israel.

Mahandaki hayo yalikuwa sehemu ya silaha muhimu kwa Palestina katika mgogoro uliodumu kwa siku 50. Katika moja ya shambulizi la kukumbukwa wanajeshi watano waliuwawa pale ambapo wapiganaji wa Hamas walipoibuka kutoka katika andaki karibu na mji wa Nahal Oz kibbutz ndani ya ardhi ya Israel, Julai 29, 2014.

Lakini mahandaki vilevile yalikuwa yakitumika ndani ya Gaza kwenyewe, pale ilipokuwa ikitokea jeshi la Israel limevamia Gaza, ambapo idadi kadhaa ya wanajeshi inadaiwa kuuwawa, baada ya wapiganaji wa Hamas kuibuka na kuwashambulio kutoka katika maandaki hayo. Kwa hivyo ripoti hii mpya ya Shapira imehitimishwa kwa kusema Netanyahu, Yaalon na mkuu wa majeshi hawakuweza kuhakikisha jeshi lina mpango mzuri wa kutekekeleza operesheni hiyo kwa ajili ya kupambana katika maeneo ya mijini yenye mahandaki.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa vita hivyo viliuwa Wapalestina 2,251 na kuwaacha wengine 100,000 bila ya makazi huku upande wa Israel watu 74 waliuwawa na sita miongoni mwa hao walikuwa wanajeshi.

Mwandishi: Sudi Mnette AFP

Mhariri: Saumu Yusuf