1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel huenda ikakubali kugawana mji wa Jerusalem na Palestina.

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CizU

Jerusalem.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kuwa nchi yake huenda ikawa haina uchaguzi bali kugawana mji wa Jerusalem na Wapalestina kama njia ya makubaliano ya amani. Olmert ameliambia gazeti la Jersalem Post kuwa hata marafiki wa Israel duniani wanaona makubaliano ya amani yakiwa kwa msingi wa mipaka ya kabla ya mwaka 1967, huku mji wa Jerusalem ukigawika. Hata hivyo Olmert amesema kuwa haoni uwezekano wa makubaliano ya kudumu chini ya mipaka ya 1967 hususan kuhusiana na eneo la ukingo wa magharibi. Israel ilikamata eneo la Waarabu la Jerusalem ya mashariki katika vita vya mwaka 1967. Wapalestina wanalitaka eneo la Jerusalem ya mashariki kuwa mji wao mkuu wa taifa lao ambalo wanataka kulianzisha katika eneo linalokaliwa na Israel la ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza.