1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Hamas zapuuza miito ya kusitisha mapigano

2 Desemba 2023

Pande za Israel na Hamas zimepuuzilia mbali miito ya kimataifa ya kuhuisha mapatano ya kusitisha mapigano ambayo muda wake umemalizika.

https://p.dw.com/p/4Zi8a
Nahostkonflikt | Chan Junis
Hali ilivyo katika maeneo ya Khan Yunis baada ya mashambulizi ya Israel.Picha: dpa

Hali hiyo inafanyika wakati mashambulizi ya anga yakielekezwa katika maeneo lengwa ya wanamgambo huko Gaza na makundi ya Wapalestina yakijibu mapigo kwa kufyatua misururu ya roketi.Moshi umeonekana kutanda tena angani kaskazini mwa ukanda wa Palestina wa Gaza, ambao serikali yake ya Hamas ilisema watu 240 wameuawa tangu kuanza tena kwa makabiliano mapema Ijumaa.Nchini Israel, Kamandi ya Jeshi imetoa taarifa ya tahadhari ya makombora 40 kwa upande wa kusini na katikati mwa nchi hiyo, na makundi ya Palestina lile laHamas na "Islamic Jihad" yametangaza mashambulio ya roketi  dhidi ya manispaa tatu za Israeli zilozo karibu na Gaza.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa inakadiriwa kuwa watu milioni 1.7 huko Gaza, takriban asilimia 80 ya jumla ya watu,  wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na vita hivi vilivyodumu kwa majuma manane sasa.