1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Palestina zaelezea matumaini yao katika mkutano wa Annapolis

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTib

ANNAPOLIS.Viongozi wa Israel na Palestina wameelezea matumaini yao ya kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili hivi karibuni.

Waliyasema hayo katika mkutano wa amani ya mashariki ya kati , huko Maryland Marekani mkutano ambao unafadhaliwa na Marekani, na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi na mashirika yapatayo 50.

Rais George Bush aliwaandalia chakula chakula cha jioni wajumbe na kuelezea matumaini yake kwa viongozi wa Israel na Palestina katika mkutano huo wa Annapolisi uliyoanza jana.

Wakati huo huo wanamgambo wawili wa Palestina na raia mmoja wameuawa na majeshi ya Israel huko katika ukanda wa Gaza.

Kundi la Hamas ambalo haliungwi mkono na Marekani limesema kuwa wapiganaji wake wawili waliuawa na majeshi hayo karibu na kambi ya Jabalya.