Israel na Palestina kuacha mapigano
27 Februari 2023Hatua hiyo inafuatiwa baada ya kuongezeka kwa machafuko mwaka huu na kusaababisha Waisraeli wawili wakiuawa katika Ukingo wa Magharibi wakati mkutano ukiendelea.
Katika taarifa yao ya pamoja baada ya mkutano huo uliofanyika eneo la Pwani la Aqaba ilisema pande zote zimekubaliana kuachana na hali ya kuhasimiana na kujitenga na machafuko zaidi.
Mazungumzo hayo ya nadra kando ya wajumbe wa Israel na Palestina kulikuwa na ushiriki wa mataifa ya Marekani na Misri.
Waisrael wawili wauwawa
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa usalama wa taifa, Itamar Ben-Gvir, walisema katika taarifa kwamba "raia wawili wa Israel waliuawa katika shambulio la kigaidi la Wapalestina" baada ya kupigwa risasi huko Huwara kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi eneo ambalo Israel inalikalia kimabavu tangu kufanyika kwa Vita vya Siku Sita vya mwaka 1967
Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake afisa mmoja wa Israel alisema ujumbe wao nchini Jordan ulijumuisha mshauri wa usalama wa taifa Tzachi Hanegbi na Ronen Bar, mkuu wa wakala wa usalama wa ndani wa Shin Bet.
Duru ya mazungumzo kuendelea
Katika muendelezo wa hatua huyo wajumbe hao duru zinaonesha wajumbe wataendelea na mazungumzo yanayojikita katika kujadili njia za kutuliza mivutano ya kiusalama katika eneo hilo kabla ya mwezi wa Ramadhani", ambao unaanza katika kipinmdi kifupi kijacho.
Vyanzo vinavyofahamu kuhusu mkutano huo vilisema mkuu wa ujasusi wa Palestina Majed Faraj pia anatarajiwa kuhudhuria.Lakini kundi la wanamgambo wa Kipalestina Hamas, ambalo linatawala Ukanda wa Gaza, liliuita mkutano huo "usio na thamani", na kulaani Mamlaka ya Palestina yenye makao yake makuu katika Ukingo wa Magharibi kwa kushiriki.
Soma zaidi:Israel yatumia ndege kushambulia Gaza
Kwa upande wake Marekani imeyapokea vyema makubalian0 hayo ya Israel na Palestina ikisema mkutano huo utakuwa ni mwanzo tu, na kwamba zipo hatua nyingi zitafuatazo katika majuma na miezi ijayo.
Chanzo: AFP