1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Jeshi la Israel lashambulia vikali eneo la kusini mwa Gaza

2 Julai 2024

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi makubwa kusini mwa Gaza na kukabiliana na wanamgambo wa Hamas, wakati jeshi hilo likiwaagiza kwa mara nyingine Wapalestina kuondoka kwenye eneo la mpaka wa Israel na Misri.

https://p.dw.com/p/4hlu4
Mzozo wa Mashariki ya Kati | Khan Younis
Wapalestina wakiwa wanaondoka katika eneo la mashariki mwa mji wa Khan Younis baada ya kuagizwa na jeshi la Israel kuondoka. Picha: Mohammed Salem/REUTERS

Mashuhuda wameripoti mashambulizi makali ya mabomu na makombora katika mji wa Khan Younis, kusini mwa mji mkuu wa Gaza ambako majeshi ya Israel yaliondoka mapema mwezi Aprili baada ya vita vikali vya miezi kadhaa.

Kulingana na chanzo cha hospitali katika mji huo, watu wanane wameuwawa na wengine 30 kujeruhiwa.

Haya yanajiri huku wakati kukiripotiwa shambulizi kwenye kambi ya wakimbizi ya Nuseirat ambapo mtoto mmoja aliuwawa, kwa mujibu wa Hilali Nyekundu ya Palestina.

Maeneo mengine ya Ukanda wa Gaza yamendelea kuathirika kutokana na mapigano ya karibu miezi tisa yaliyochochewa na shambulio la Hamas la Oktoba 7 dhidi ya Israel.