Israel tayari kupatanisha mzozo wa Urusi na Ukraine
1 Februari 2023Matangazo
Netanyahu alisema hayo kwenye mahojiano yaliyorushwa siku ya Jumanne (Januari 31, lakini hakutoa ahadi madhubuti kwa Ukraine.
Israel imehifadhi uhusiano wake na Urusi, ambayo inadhibiti anga ya taifa jirani la Syria, nayo Urusi imefumbia macho mashambulizi ya angani yanayofanywa na Israel dhidi ya Iran, mshirika muhimu wa Moscow kwenye eneo la Mashirika ya Kati.
Kwenye mahojiano hayo na kituo cha televisheni cha CNN cha Marekani, Netanyahu aliulizwa ikiwa angelitoa msaada kama vile mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora chapa Iron Dome kwa Ukraine, naye akajibu kwa kusema angali anatafakari kuhusu hilo.
Mfumo huo wa kiteknolojia unaoungwa mkono na Marekani huilinda Israel dhidi ya mashambulizi ya kutokea angani.