1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaidhinisha ujenzi wa makaazi mapya

12 Agosti 2013

Israel imetoa orodha ya wafungwa 26 wa Kipalestina watakaochiliwa huru kama sehemu ya mpango wa kuufufua mchakato wa amani. Pia imeidhinisha ujenzi wa zaidi ya nyumba mpya 1,200 katika makaazi ya Kiyahudi

https://p.dw.com/p/19NsS
Houses are seen in the West Bank Jewish settlement of Ofra, north of Ramallah July 18, 2013. Negotiations between Israel and the Palestinians, which have ebbed and flowed for two decades, last broke down in late 2010, after a partial settlement halt meant to foster talks ended and Israeli Prime Minister Benjamin Netanyahu refused to extend it. Palestinians familiar with Palestinian President Mahmoud Abbas' thinking speculated he might now forgo the demand for a settlement moratorium given a recent slowdown in housing starts issued by Israel's government, though it may still be painful to roll back his previous demand. If Abbas yields on the issue, it may be in exchange for a goodwill gesture from Israel such as amnesty for around 100 veteran PLO fighters long held in its jails. REUTERS/Baz Ratner (WEST BANK - Tags: POLITICS CIVIL UNREST BUSINESS CONSTRUCTION)
Westjordanland israelische Siedlung Ofra bei RamallahPicha: Reuters

Tangazo la Israel la kuidhinisha ujenzi wa makaazi mapya ya kiyahudi na kuwaachia huru wafungwa wa Kipalestina limekuja kabla ya kuanza tena mazungumzo ya ana kwa ana baina ya Israel na mamlaka ya ndani ya Palestina mjini Jerusalem, Jumatano wiki hii.

Wizara ya makaazi ya Israel imesema nyumba 1,187 zimeidhinishwa ambapo zaidi ya nusu zitajengwa katika Jerusalem ya Mashariki, ambayo ilinyakuliwa na Israel mara tu baada ya vita vya mwaka wa 1967, hatua ambayo haitambuliwi na jumuiya ya kimataifa.

Mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yanaanza tena Jumatano, mjini Jerusalem
Mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina yanaanza tena Jumatano, mjini JerusalemPicha: AFP/Getty Images

Nyumba nyingine zitajengwa katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi ya Maaleh Adumin, Efrat na Ariel. Duru ya kwanza ya mazungumzo baina ya Waisrael na Wapalestina ilifanyika mjini Washington mwishoni mwa mwezi wa Julai, baada ya kukwama kwa karibu miaka mitatu.

Mjumbe mkuu wa Palestina Saed Erakat amesema kuwa tangazo hilo la ujenzi wa nyumba mpya ni “ushahidi wa wazi” kuwa serikali ya Israel “haijajitolea kwa ajili ya mazungumzo hayo”. Erakat amesema "Tunaiomba serikali ya Israel ikomeshe ujenzi wa makaazi haya na kuupa nafasi inayostahili mchakato wa amani ili kupatikana suluhisho la mataifa mawili"

Waziri wa Mambo ya Nchi za Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle yuko katika eneo hilo, na hapo jana amekutana na Mjumbe wa Israel Tzipi Livni ambapo aliupinga ujenzi huo. Westerwelle amesema "Hatutaki upande wowote uchukue hatua zozote zinazoweza kuhujumu mazungumzo haya na sisi tutakeleza jukumu muhimu katika mazungumzo haya" Kundi la wanaharakati wa Israel, la Amani Sasa yaani Peace Now, limesema hatua hiyo itakuwa kikwazo kikubwa kwa mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle na mjumbe wa Israel Tzipi Livni
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle na mjumbe wa Israel Tzipi LivniPicha: picture-alliance/dpa

Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas, amesisitiza kwa muda mrefu kuwa hapawezi kuwepo na mazungumzo bila kusitishwa ujenzi wa makaazi ya wayahudi. Lakini makubaliano yalifikiwa ya kuanzisha tena mazungumzo baada ya Israel kusema kuwa itawaachia zaidi ya wafungwa 100 maveterani wa Kipalestina.

Wakati huo huo, Idara ya Magereza ya Israel imetoa majina ya wafungwa hao 26 mapema leo kwenye mtandao wa internet, ili kuruhusu siku mbili za kuwasilisha kesi zozote za rufaa mahakamani. 21 kati yao walihukumiwa kwa mashitaka ya mauwaji, ikiwa ni pamoja na Waisrael na washukiwa wa Kipalestina walioshirikiana nao, wakati wengine wakihusika na matukio ya kujaribu kuua au utekaji nyara.

Nusu ya wafungwa kwenye orodha hiyo hawakuwa na tarehe ya kuwachiliwa huru, maana kuwa walikuwa wakitumikia vifungo vya maisha jela, wakati wengine wangeachiliwa katika miaka michache ijayo bila mpango maalum. Wengi tayari wametumikia miaka 20.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP

Mhariri: Daniel Gakuba