1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kujadili kwa mara nyingine hatua dhidi ya Iran

16 Aprili 2024

Baraza la mawaziri la Vita la serikali ya Israel linatarajiwa kukutana tena kujadili hatua za kuchukua kujibu shambulizi la mwisho wa juma la Iran dhidi ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4erHm
Baraza la mawaziri la Vita la serikali ya Israel.
Baraza la mawaziri la Vita la serikali ya Israel likiwa katika kikao chake baada ya shambulio la Iran.Picha: Israeli Government Press Office/Anadolu/picture alliance

Hiyo itakuwa mara ya tatu baraza hilo linakutana, mnamo wakati shinikizo la kimataifa linaongezeka la kuepusha hatua yoyote inayoweza kuzidisha mzozo katika Mashariki ya Kati.

Ingawashambulio la Iran lilisababisha uharibifu mdogo tu, na halikusababisha kifo, limeongeza wasiwasi wa uwezekano wa vita vya Gaza kutanuka zaidi na hofu ya kuanza kwa vita kati ya mataifa hayo mawili ambayo ni maadui wa muda mrefu.

Soma pia:Iran yaipa onya kali Israel isijaribu kujibu mashambulizi

Mnamo mwishoni mwa Juma, Rais wa Marekani Joe Biden alimwambia Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kwamba Marekani ambayo ni mlinzi mkuu wa Israeli, haitashiriki katika shambulio la kulipiza kisasi dhidi ya Iran.