Israel yajiandaa kuidhinisha makubaliano ya kusitisha vita
17 Januari 2025Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Baraza la mawaziri nchini Israel litakutana kwa ajili ya kutoa idhini ya mwisho ya makubaliano na kundi la Hamas ya kusitisha mapigano huko Ukanda wa Gaza na kuwaachilia mateka.
Soma: Ofisi ya Netanyahu yakanusha Hamas kukubali pendekezo la kusitisha vita
Ofisi ya waziri mkuu huyo imesema mapema leo kwamba wanakaribia kutoa idhini hiyo na baraza la Usalama litakutana kabla ya mkutano wa Baraza kamili la mawaziri ili kuidhinisha makubaliano hayo.
Haya yanaelezwa katikati ya wasiwasi kwamba makubaliano hayo huenda yakacheleweshwa kufuatia madai ya Israel hapo jana kwamba Hamas wanajaribu kuyazuia. Vifo Gaza vyaongezeka hadi 77 tangu makubaliano yalipofikiwa
Bado haijulikani kama baraza hilo litakutana leo ama kesho Jumamosi ama hata ikiwa kutakuwa na ucheleweshwaji wa usitishwaji wa mapigano, uliotarajiwa kuanza siku ya Jumapili.