1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imemuua kamanda wa ngazi ya juu wa Hezbollah

4 Novemba 2024

Jeshi la Israel limesema leo kwamba limemuua kamanda wa ngazi ya juu wa kundi la Hezbollah linayemtuhumu kuratibu mashambulizi ya maroketi dhidi vikosi vya Israel kusini mwa Lebanon.

https://p.dw.com/p/4mZBf
Lebanon | Mashambulizi ya Israel dhidi ya Hezbollah
Mashambulizi ya Israel nchini Lebanon yameuwa takribani watu 2,000 katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja.Picha: KAWNAT HAJU/AFP

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo limesema, Abu Ali Rida, kamanda wa Hezbollah kwenye eneo la Baraachit, kusini mwa Lebanon "ameuawa" katika shambulizi la anga. 

Jeshi la Israel limesema Rida alikuwa akiongoza shughuli za kigaidi ikiwa ni pamoja na kupanga mashambulizi yaliyowalenga wanajeshi na zana za kivita za Israel kusini mwa Lebanon. 

Soma pia:Matumaini ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hezbollah 

Mauaji ya Rida yametangazwa wakati Israel inaendelea kuzishambulia ngome za kundi la Hezbollah ndani ya Lebanon katika kampeni yake ya kijeshi iliyoanza mwezi Septemba. 

Kwa upande mwengine, kundi la Hezbullah limesema kuwa limerusha mkururo wa maroketi kuelekea mji wa Safed kaskazini mwa Israel mapema hivi leo.