1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imeruhusu msaada zaidi kuingia Gaza

Hawa Bihoga
20 Aprili 2024

Israel imearifu kuongeza juhudi za kuingiza misaada ya kiutu kwa wakaazi wa Gaza ambapo malori 276 yaliyobeba chakula na dawa yaliwasili Ukanda wa Gaza, mamlaka inayohusika na mawasiliano na Wapalestina, COGAT, imesema.

https://p.dw.com/p/4f01s
Malori yanayojiandaa kuingia Ukanda wa Gaza yakiwa na misaada ya kiutu
Malori yanayojiandaa kuingia Ukanda wa Gaza yakiwa na misaada ya kiutuPicha: Israeli Army via AFP

Aidha, paleti 144 za chakula zilidondoshwa kutokea angani, na malori mengine 700 yanasubiri nyuma ya kituo cha ukaguzi cha Kerem Shalom, tayari kuchukuliwa na mashirika ya msaada ya Umoja wa Mataifa ya kusambaza chakula. 

Kutokana na janga la kibinadamu linalowatishia watu wa Gaza, Israel imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka washirika wake wa magharibi na Umoja wa Mataifa, kuitaka iruhusu haraka kuingizwa kwa shehena zaidi za msaada. 

soma pia:UNRWA lasema hakuna mabadiliko makubwa kuhusu misaada inayoingia Gaza

Ingawa mashirika ya wahisani yametambua ongezeko la msaada unaoingia Gaza, yanasisitiza kuwa bado malori yanayoruhusiwa kuingia hayatoshi, na kulalamika kuwa mapigano yanayoendelea yanakwamisha usambazaji wa msaada unaowasilishwa.