1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Baadhi ya Walebanon washindwa kurejea katika makazi yao

29 Novemba 2024

Msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee, amesema leo kuwa wakazi wa Lebanon wamepigwa marufuku kuhamia katika eneo la kusini kwenye baadhi ya vijiji na viunga vyake hadi itakapoarifiwa tena.

https://p.dw.com/p/4nYlk
Benjamin Netanyahu
Benjamin NetanyahuPicha: Maayan Toaf/Israel Gpo/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Msemaji wa jeshi la Israel Avichay Adraee, amesema leo kuwa wakazi wa Lebanon wamepigwa marufuku kuhamia katika eneo la kusini kwenye baadhi ya vijiji na viunga vyake hadi itakapoarifiwa tena.

Katika chapisho lake la hivi karibuni, Adraee alitoa wito kwa wakaazi wa Lebanon kutorejea katika zaidi ya vijiji 60 vya eneo la kusini, na kuongeza kuwa mtu yeyote atakayekiuka agizo hilo atakuwa anahatarisha maisha yake.

Hapo jana, majeshi ya Israel yalifyatua risasi dhidi ya kile ilichosema ni washukiwa waliokuwa na magari wakielekea katika maeneo hayo yaliopigwa marufuku na ikaitaja hatua hiyo kuni ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano kutoka kwa kundi la Hezobollah.

Kwa upande wake, mbunge wa Hezbollah Hassan Fadlallah ameishtumu Israel kwa kukiuka makubaliano hayo.

Fadlallah amewaambia waandishi wa habari kwamba Israel inawashambulia watu wanaorejea katika vijiji vya mpakani, na kuongeza kuwa kwa hatua hiyo, Israel imekiuka makubaliano hayo.