MigogoroLebanon
Israel yashambulia njia za kusafirisha silaha kwa Hezbollah
13 Januari 2025Matangazo
Shirika la habari la serikali ya Lebanon limeripoti kuwa, Israel imeshambulia maeneo ya mji wa Janta katika mkoa wa mashariki wa Baalbek pamoja na maeneo ya kusini karibu na Nabatieh. Hata hivyo, hakukuwepo ripoti zozote za majeruhi.
Soma pia: IDF lashambulia "miundombinu ya kijeshi" ya Hezbollah, likisema wanakiuka makubaliano
Jeshi la Israel limeeleza kwamba limezilenga ngome za kundi la wanamgambo la Hezbollah ikiwa ni pamoja na njia za magendo zinazotumiwa kusafirisha silaha kandokando mwa mpaka na Syria.
Mashambulizi hayo yanaongeza mashaka juu ya mpango dhaifu wa usitishaji mapigano kati ya Israel na Hezbollah ambao ulianza kutekelezwa kuanzia Novemba 27.