1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatarajiwa kukubali usitishaji vita na Hezbollah

26 Novemba 2024

Israeli inaonekana kuwa tayari kupitisha mpango wa Marekani wa kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah. Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu wa Israel.

https://p.dw.com/p/4nQoR
Uharibifu wa jengo mjini Beirut | Lebanon
Uharibifu wa jengo mjini BeirutPicha: AFP

Israeli inaonekana kuwa tayari kupitisha mpango wa Marekani wa kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah. Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu wa Israel.

Soma kwa kina kuhusu makubaliano hayo: Israel na Lebanon zakubali masharti ya kusitisha vita

Baraza la usalama la Israel linatarajiwa kukutana baadaye leo Jumanne ili kujadili na pengine kuidhinisha kwa mpango huo kwenye mkutano unaoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Mkataba huo tayari umeidhinishwa mjini Beirut, ambako Naibu spika wa bunge la Lebanon ameliambia shirika la habari la Reuters hapakuwa na vikwazo vizito vilivyosalia vitakavyozuia makubaliano hayo kuanza kutekelezwa, labda Netanyahu abadili mawazo.

Naibu spika wa bunge la Lebanon, Elias Bou Saab amesema mpango huo unawataka wanajeshi wa Israel kuondoka kusini mwa Lebanon na wanajeshi wa Lebanon kupelekwa katika vikosi vyake katika eneo la mpaka, ngome ya Hezbollah ndani ya siku 60.