ISTANBUL: Gul ateuliwa tena kugombea urais
14 Agosti 2007Matangazo
Chama tawala nchini Uturuki cha AK kimemteua tena waziri wa mashuri ya kigeni, Abdullah Gul, kuwa mgombea wake kwenye uchaguzi wa rais utakaofanyika wiki ijayo.
Uteuzi wa Gul mwezi Aprili mwaka huu ulisababisha maandamano makubwa kwenye miji mikubwa nchini Uturuki na kukilazimisha chama cha AK kilicho na misingi ya dini ya kiislamu kikiongozwa na waziri mkuu, Recep Tayyip Erdogan, kiitishe uchaguzi wa mapema.
Waturuki wasio na msimamo mkali wa kidini, wakimwemo pia majenerali wa jeshi la Uturuki, wanahofia chama cha AK kinapania kuvuruga utulivu uliopo baina ya taifa na dini katika nchi hiyo iliyo na idadi kubwa ya waislamu. Chama cha AK kimeendelea kupinga madai hayo.