1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Majirani wakubali kuisaidia Iraq

1 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFHm

Majirani wa Iraq wametoa hati ya pamoja wakiiunga mkono serikali mpya ya Baghdad.Mwishoni mwa majadiliano yao katika mji wa Istanbul,majirani hao wameahidi kuimarisha ushirikiano katika uwanja wa usalama,kwa lengo la kuwazuia wanamgambo kuingia nchini Iraq.Baghdad imezituhumu Syria na Iran kuwa zinawaruhusu wapiganaji wa kigeni kuvuka mipaka.Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan,alionya kuwa utulivu wa Iraq ni suala linaloihusu kanda nzima.Erdogan akaongezea kuwa angependa kuyaona mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za Kiarabu yakishiriki zaidi kwa vitendo nchini Iraq.Mbali na nchi sita zinazopakana na Iraq yaani Uturuki, Iran,Kuwait,Saudi Arabia,Jordan na Syria mkutano huo ulihudhuriwa pia na wajumbe kutoka Misri na Bahrain.