ISTANBUL : Merkel akamilisha ziara Uturuki
7 Oktoba 2006Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekamilisha ziara yake nchini Uturuki ambapo amesisitiza umuhimu wa uhusiano wa kibishara na nchi hiyo lakini hakuunga mkono harakati za Uturuki za kutaka kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Amesema mageuzi yaliotekelezwa na Uturuki hadi sasa tayari yameinuwa uchumi wake.Merkel ambaye chama chake cha kihafidhina nchini Ujerumani kinataka Utruruki kuwa mshirika maalum tu kwa Umoja wa Ulaya amesema Uturuki na Umoja wa Ulaya zote zinapaswa kujiepusha na vikwazo zaidi katika mzozo wao juu ya uhusiano wa biashara na Cyprus.
Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kwamba Umoja wa Ulaya uondowe vikwazo kwa upande wa kaskazini wa kisiwa hicho kilichogawika chenye asili ya Uturuki. Uturuki inakataa kufunguwa bandari zake na viwanja vya ndege kwa Cyprus venginevyo Umoja wa Ulaya nao pia unafanya hivyo.
Merkel na Erdogan baadae walikutana na viongozi wa Kiislam na Wakristo wa madhehebu ya Orthodox.