Istanbul. Mkutano wapangwa kufanyika licha ya upinzani wa mahakama.
24 Septemba 2005Mkutano kuhusiana na mauaji ya Warmenia chini ya himaya ya Ottoman kiasi cha miaka 100 iliyopita utafanyika mjini Istanbul licha ya kupigwa marufuku na mahakama.
Mkutano huo una lengo la kuangalia kwa undani matukio hayo ya mwaka 1915.
Uturuki inakana madai ya Waarmenia kuwa zaidi ya watu milioni 1.5 waliuwawa katika mauaji ya halaiki.
Mahakama moja nchini Uturuki imesitisha mkutano huo unaotarajiwa kufanyika siku ya Alhamis kufuatia malalamiko ya wazalendo kuwa watayarishaji wa mkutano huo ni wasaliti.
Lakini chuo kikuu cha tatu kimejitokeza kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na mshikamano na vyuo vingine viwili vilivyojitokeza kuwa wenyeji wa mkutano huo. Hii inakwenda kinyume na amri ya mahakama hiyo, ambayo imepiga marufuku mkutano huo kufanyika.
Umoja wa Ulaya umeshutumu vikali uamuzi huo wa mahakama.