1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul. Mtuhumiwa wa mauaji akamatwa.

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZD

Mtuhumiwa mkuu katika mauaji ya mwandishi habari wa Uturuki mwenye asili ya Armenia Hrant Dink amekamatwa na polisi wa Uturuki. Mtuhumiwa huyo Ogun Samas , anaripotiwa kuwa amekamatwa usiku wa Jumamosi katika basi karibu na bandari iliyoko katika bahari Nyeusi wa Samsun.

Polisi walitoa picha na video za mtuhumiwa huyo mapema jana Jumamosi.

Dink mwenye umri wa miaka 53 alipigwa risasi na kufariki siku ya Ijumaa nje ya ofisi yake mjini Istanbul ya gazeti la Agos. Wazalendo wa Kituruki wamekasirishwa na maelezo ya Dink kuwa ni mauaji ya halaiki mauaji ya Warmenia yaliyofanywa wakati wa utawala wa Ottoman katika Uturuki kati ya mwaka 1915 na 1918.

Katika makala yake ya mwisho, Dink amesema kuwa amepokea vitisho vya kuuwawa kutoka kwa wazalendo hao. Mauaji yake yamezusha shutuma kali kote duniani na maandamano nchini Uturuki.