ISTANBUL: Rais wa Uturuki apinga mapendekezo ya kurekebisha katiba
26 Mei 2007Matangazo
Rais wa Uturuki, Ahmet Necdet, kama ilivyotarajiwa, amepinga kwa kura ya turufu mabadiliko yaliyopendekezwa ya katiba kwamba rais anayefuata wa nchi hiyo achaguliwe moja kwa moja na wapiga kura badala ya bunge.
Chama tawala cha AK, kilicho na misingi ya Kiislamu, kilipitisha mapendekezo hayo mapema mwezi huu baada ya wabunge wanaopinga utawala wa kidini kususia uchaguzi wa urais.
Watu wanaopinga utawala wa kidini nchini humo ambao wanaungwa mkono na wanajeshi, wanadai katiba hairuhusu kuwepo kwa waziri mkuu na rais walio na misingi ya Kiislamu.
Uchaguzi wa urais umeahirishwa mpaka baada ya uchaguzi mkuu wa mapema wa tarehe 22 mwezi Julai.