Istanbul. Uturuki. Papa Benedict asali msikitini.
1 Desemba 2006Kiongozi wa kanisa Katoliki Pope Benedict ametembelea msikiti maarufu wa kibuluu akisindikizwa na kiongozi mwandamizi wa dini ya Kiislamu , mufti mkuu wa mji huo Mustafa Cagrici.
Walisali pamoja katika msikiti huo. Hii inamfanya Pope Benedict kuwa kiongozi mkuu wa pili wa kanisa Katoliki kuingia msikitini.
Makao makuu ya Papa ya Vatikan yameionyesha ziara hiyo ya papa kuwa ni ishara ya heshima kwa Waislamu, lakini imesababisha upinzani kwa Waislamu kadha wenye msimamo mkali.
Hapo mapema , Papa alitembelea sehemu nyingine muhimu mjini Istanbul, inayojulikana kama Aya Sofya.
Jengo hilo kwanza lilikuwa kanisa la wakati wa enzi za ufalme wa Byzantine wa Ugiriki, baadaye likawa msikiti na sasa ni makumbusho.
Katika ziara hiyo alikuwa na gavana ya jiji la Istanbul.
Papa Benedict pia alikuwa na mazungumzo na kiongozi wa kanisa la Kiothodox bartholomew 1.
Papa katika mazungumzo hayo alitoa wito kwa Wakristo.
Viongozi hao wa kidini waliongeza kuwa haki za walio wachache zinapaswa kulindwa wakati umoja wa Ulaya unazidi kupanuka.