Istanbul. Uturuki yashambuliwa kwa bomu.
11 Julai 2005Matangazo
Kiasi cha watu 20 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu katika eneo maarufu la kitalii magharibi ya Uturuki.
Bomu hilo linasemekana liliwekwa katika pipa la kutupia taka karibu na benki katika mji wa Cesme ulioko katika jimbo la Izmir.
Maafisa wamesema kuwa watu wawili , raia wa kigeni ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa.
Wataalamu wa mabomu bado wanachunguza eneo la tukio na polisi wamelifunga kabisa eneo hilo.
Hakuna kikundi kilichodai kuhusika na tukio hilo hadi sasa.
Hapo kabla , wapiganaji wa Kiislamu na kundi la Wakurdi wanaotaka kujitenga wamekuwa wakihusika na mashambulizi ya mabomu nchini Uturuki.