Istanbul yapigwa na tetemeko la ardhi
4 Desemba 2023Matangazo
Kitovu cha tetemeko hilo ni katika ukanda wa pwani wa Gemlik ulio kwenye Bahari ya Marmara umbali wa takriban kilomita 60 kusini mwa Istanbul.
Kulingana na Idara ya Huduma za Dharura ya Uturuki (AFAD, ettemeko hilo halikusababisha uharibifu wowote na pia hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Soma zaidi: Idadi ya watu waliokufa kutokana na mitetemeko ya ardhi yapindukia 25,000 nchini Uturuki na Syria.
Kituo cha Utafiti wa Jiologia cha nchini Ujerumani (GFZ) kilisema tetemeko hilo lilikuwa na kasi ya takribani kilomita 10 kwa saa.