1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIvory Coast

Ivory Coast yawataka wanajeshi wa Ufaransa kuondoka

1 Januari 2025

Ivory Coast imetangaza kuwa wanajeshi wa Ufaransa wataondoka nchini humo baada ya kuwepo huko kwa miongo kadhaa. Ni taifa la karibuni la Kiafrika kupunguza uhusiano wa kijeshi na mtawala wake wa zamani.

https://p.dw.com/p/4oiqC
Askari wa Ufaransa wakishika doria katika mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan
Ufaransa ina hadi askari 600 nchini Ivory CoastPicha: picture alliance/dpa

Ufaransa ina hadi askari 600 nchini Ivory Coast. Tangazo la Ouattara linafuatia la viongozi wengine wa Afrika Magharibi, ambako majeshi ya Ufaransa yanatakiwa kuondoka.

Wakati huo huo, Rais wa Senegal Bassirou Dioumaye Faye amesema kuwa wanajeshi wote wa kigeni wataondoka nchini humomwaka huu. Katika hotuba ya kuukaribisha mwaka mpya, Faye amesema amemuagiza waziri anayesimamia wanajeshi kutayarisha mkataba mpya wa ushirikiano katika ulinzi na usalama. Faye alisema mwezi mmoja uliopita kuwa mtawala wake wa zamani Ufaransa atahitajika kufunga kambi zake za kijeshi nchini Senegal. Lakini hii ni mara ya kwanza ameweka tarehe ya kufungwa kwa vituo vyote vya majeshi ya kigeni.

Ufaransa imekumbwa na misukosuko kama hiyo katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi katika miaka ya karibuni, zikiwemo Chad, Niger na Burkina Faso, ambako wanajeshi wa Ufaransa waliokuwa katika nchi hizo kwa miaka mingi wamefukuzwa.