Jaji asema polisi nchini Kenya wana kesi ya kujibu
20 Septemba 2021Matangazo
Wakili Willie Kimani na mteja wake Josephat Mwendwa walitoweka Juni mwaka 2016, muda mfupi baada ya kufungua kesi kudai kuwa Mwendwa amepigwa risasi na kujeruhiwa na polisi.
Siku chache baadae miili yao pamoja na ya dereva taksi Joseph Muiruri ilipatikana kwenye mto nje kidogo ya Nairobi.
Wanaume wote hao watano awali walikana mashtaka. Wakili wao hakupatikana kuzungumzia suala hilo.
Kimani alikuwa akifanya kazi na shirika la kimataifa la kutetea haki ambalo limeufurahia uamuzi huo wa Jaji Lessit.
Washtakiwa katika kesi hiyo watawasilisha utetezi wao Septemba 27 katika hatua inayofuata ya kesi hiyo.