Sullivan yupo Saudia kujadili hali ya Mashariki ya Kati
18 Mei 2024Matangazo
Kulingana na msemaji wa Baraza la usalama la taifa nchini Marekani Jon Kirby, Jake Sullivan atakutana na mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman kujadili juhudi za kupatikana amani na usalama wa kanda nzima ya Mashariki ya kati.
Siku ya Jumapili Sullivan atasafiri kuelekea Israel atakakokutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
'Israel laazima izuwiwe', Afrika Kusini yaiambia ICJ
John Kirby amesema mazungumzo yao yatatuwama katika masuala ya vita katika ukanda wa Gaza, hali ya kibinaadamu huko na majadiliano juu ya makubaliano ya kuwaachia mateka wanaoshikiliwa na kundi la wanamgambo wa Hamas.