DRC kuanza kutoa chanjo ya Malaria Jumanne
25 Oktoba 2024Matangazo
Kwa mujibu wa shirika hilo, itakuwa ni mara ya kwanza kwa Wizara ya Afya ya nchi hiyo kutoa chanjo ya malaria. Chanjo za awali zitatolewa katika mkoa wa Kongo Kati, ulio Kusini Magharibi mwa nchi. Kulingana na WHO, awamu ya kwanza ya dozi zaidi ya laki sita ziliwasili mwezi Juni. Aina hiyo ya chanjo imeshatumika katika nchi nyingine za Afrika zikiwemo Kenya, Cameroon, Malawi na Benin. Ugonjwa wa Malaria unaoweza kusababisha kifo huambukizwa kwa binadamu kupitia mbu na miongoni mwa dalili zake ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa pamoja na homa ya manjano. Watoto wa umri wa chini ya miaka mitano ndio hufariki zaidi kwa Malaria.