1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Japan yalaani vitisho vya Urusi vya nyuklia

6 Agosti 2023

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida amelaani vitisho vya Urusi vya kutumia silaha za nyuklia wakati nchi hiyo ikifanya kumbukumbu ya miaka 78 tangu shambulizi la bomu la atomiki kwenye mji wa Hiroshima

https://p.dw.com/p/4Up3V
Japan, Hiroshima | 78. Jahrestag des Atombombenabwurf
Picha: AP/Kyodo News/picture alliance

Kishida amesema katika hafla hiyo mjini Hiroshima kuwa Japan, kama taifa pekee lililopigwa na mabomu ya atomiki wakati wa vita, itaendeleza juhudi za kuwa na ulimwengu usiokuwa na zana za nyuklia.

Amesema mkondo wa kufikia lengo hilo unaendelea kuwa mgumu kwa sababu ya migawanyiko mikubwa inayoshuhudiwa katika jamii ya kimataifa kuhusu kupunguza au kuondoa silaha za nyuklia na kitisho cha Urusi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kutokana na vitisho vya baadhi ya madola, jamii ya kimataifa lazima izungumze kwa sauti moja. Karibu watu 140,000 walifariki mjini Hiroshima Agosti 6, 1945 na 74,000 mjini Nagasaki siku tatu baadae, wakati Marekani ilipodondosha mabomu ya atomiki kwenye miji hiyo miwili ya Japan siku chache kabla ya kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.