Mabadiliko ya sayari yamesababisha changamoto kubwa katika bahari, hata baadhi ya viumbe wapo hatarini kutoweka kando na hilo uvuvi haramu ni changamoto nyingine inayotishia maisha yao, sasa kutana na Stella masai anatoa elemu kwa jamii ili kunusuru viumbe baharini.
Kipindi hiki kinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Msichana Jasiri ni muwazi, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!