Chini ya mwaka 1 wapigakura nchini Tanzania, watakuwa wamepiga kura zao kwenye uchaguzi mwengine mkuu unaotazamiwa kuvishirikisha vyama vingi. Tayari joto la uchaguzi limeshashika kasi miongoni mwa rubaa za kisiasa na wadau wengine kwenye taifa hilo. Lakini je, miaka minne ya utawala wa Rais Magufuli imekuwa na maana gani hadi sasa kuelekea uchaguzi huo? Mohammed Khelef anaongoza mjadala huo.