1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Pakistan ni msaidizi au kikwazo kwa vita dhidi ya ugaidi?

8 Agosti 2011

Kiongozi wa Al-Qaeda Osama Bin Laden alijificha Abottabad,Pakistan kwa miaka kingi. Hiyo imezusha suala kuhusu uaminifu wa Pakistan kama mshirika wa nchi za Magharibi.

https://p.dw.com/p/Re1w
--- DW-Grafik: Simone Hüls 911_AB_pakistanusa 911_pakistanusa_MB
Picha: AP/DW

Maficho ya Osama bin Laden huko Abottabad nchini Pakistan yamezusha masuala kadhaa. Je, nchi hiyo ni mshirika anayeaminika? Je, inawapinga Taliban na al-Qaida nchini Afghanistan?

Wataalamu wengi wanasema, jawabu ni "la". Kwa maoni yao, Pakistan inayoshindana na hasimu wake mkuu, India, inacheza mchezo wa hatari pande mbili. Mara kwa mara, Marekani hueleza hadharani kuwa Pakistan ni mshirika wake. Katika miaka ya ’80, mataifa haya yalikuwa washirika mpaka majeshi ya Kirusi yalipoondoka Afghanistan. Hapo Marekani haikuwa na utashi tena. Lakini kufuatia mashambulio ya Septemba 11, Pakistan ikawa na umuhimu kama nchi ya kusafirisha mahitaji ya majeshi ya kimataifa yanayopigana dhidi ya Taliban na al-Qaida nchini Afghanistan. Mtaalamu wa masuala ya Asia ya Kusini, Conrad Schetter, anasema Pakistan ilikubali shingo upande. "Utashi mwingine wa Pakistan hasa ni kuona hali mbaya ikiendelea nchini Afghanistan. Inachotaka huko Afghanistan ni serikali inayoridhisha maslahi ya Pakistan."

Pakistan inataka kujadiliana na sio kuwashinda Taliban

Kwa maneno mengine, Pakistan haina hamu ya kuchukua hatua kali dhidi ya washirika wake wa zamani, Taliban. Kwani mkakati ni majeshi yake kuwa na kimbilio huko Afghanistan iwapo itapigana vita na jirani yake, India. Pakistan na India, ambazo zote zinamiliki silaha za nyuklia, zimeshapigana vita mara tatu bila ya kupata ufumbuzi wa mgogoro wao wa mpakani.

Dreiergipfel-Washington.jpg
Hakuna uhusiano wa urahisiPicha: AP

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya ugaidi, Rahimullah Yusufzai, mkakati wa serikali ya Pakistan ni kujaribu kuwa na ushirikiano wa karibu na makundi ya Kiislamu. "Tofauti za maoni kati ya Pakistan na Marekani, hali kadhalika nchi zingine za Magharibi, zinasababishwa na sera zake kuhusiana na Taliban. Pakistan inajitahidi kupata ufumbuzi wa kisiasa na inataka kujadiliana na Taliban. Vile vile inataka kuwa na usemi katika majadiliano hayo. Lakini azma ya Marekani ni kuwashinda Taliban." Anasema Yusufzai.

Hata hivyo, Marekani pia sasa ipo tayari kwa majadiliano kwa sharti la kwanza Taliban kujitenga na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida. Marekani ina kiasi ya wanajeshi 100,000 nchini Afghanistan kuwashinikiza Wataliban kuingia katika majadiliano ya amani. Hata maficho ya wanamgambo wake nchini Pakistan yanashambuliwa na ndege zisizo na rubani. Ujumbe wa Marekani ni dhahiri: Ushirikiano kati ya Pakistan na magaidi hautostahmiliwa. Lakini wataalamu wa masuala ya kisiasa wana shaka iwapo serikali ya Pakistan itaweza kubadili kabisa mkondo wa sera zake kuhusu Taliban. Jeshi la Pakistan lina nguvu na idara ya upelelezi ina ushawishi mkubwa.

Pakistan yacheza timu zote mbili kwenye mechi moja

Islamic militants are seen during training in the Pakistani territory near Afghanistan border in this undated image from video provided by the Indian security agencies in New Delhi Monday, Sept.17, 2001. According to intercepts provided by Indian security officials in Kashmir, members of the Pakistan-based Hezb-ul Mujahedeen guerrilla group sang into radio transmitters on Friday night from a mountainous area in Pakistan-controlled Kashmi in praise of Osama bin Laden. Videotapes in the hands of American investigators show several Islamic militants in mountain camps in Pakistan, near the Afghanistan border, firing automatic rifles and grenade and rocket launchers as they swing on ropes through trees and slide down from lofty heights. (AP Photo/Video Courtesy Indian Security Agencies)
Shinikizo kubwa kwa serikali inaweza ikapendelea vikosi vya KiislamuPicha: AP

Pakistan haitaki kukosa msaada wa mabilioni ya dola unaotolewa na Marekani kila mwaka. Bali pia serikali ya Islamabad inataka kudumisha uhusiano wake mzuri na makundi yenye itikadi kali ndani ya Afghanistan. Kwa hivyo, Pakistan inacheza pande zote mbili za mechi hii. Lakini Marekani haitaki tena kuvumilia mchezo huo. Juu ya hivyo, Hennig Riecke, mtaalamu wa Kimarekani kwenye Jumuiya ya Kijerumani ya Sera za Kigeni (DGAP) anasema, serikali ya Marekani itahitaji subira kubwa "kuishawishi Pakistan kufikiria upya."

Katika vita vya Afghanistan dhidi ya Taliban na al-Qaida, Marekani na Pakistan zina maslahi tofauti na wakati huo huo zinaendelea kutegemeana katika ushirikiano wenye utata.

Mwandishi: Ratbil Shamel/ZPR

Tafsiri: Prema Martin