Ukiamka asubuhi kitu cha kwanza unafanya nini? Wengi tunaangalia simu ya mkononi. Na tunajua hatupo peke yetu. Tukiamka tu tunaangalia nani katutumia ujumbe mfupi katika Whatsapp, wakati tulipokuwa tumelala. Simu za mkononi zimekuwa sehemu kubwa sana ya maisha yetu, jambo linaloipa wasiwasi jamii. Kuna programu za kusaidia kupunguza matumizi ya simu..