1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem. Annan aitaka Israel kuacha kuizingira Lebanon.

30 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDGp

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amekutana mjini Jerusalem na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert. Annan anajaribu kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na umoja wa mataifa ambayo yamemaliza mapigano yaliyodumu zaidi ya mwezi mmoja baina ya majeshi ya Israel na wapiganaji wa Hizbollah.

Viongozi hao wawili walijadili uwekaji wa majeshi zaidi ya umoja wa mataifa kusini mwa Lebanon, na Annan amemtaka waziri mkuu Olmert kuondoa hatua ya kuzingira Lebanon katika anga yake, ardhini na baharini.

Hata hivyo , katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kufuatia mkutano wao, Olmert ameepuka suala la kuizingira Lebanon, na akarudia kuwa majeshi ya ulinzi ya Israel yatarudishwa nyumbani wakati majeshi ya umoja wa mataifa yatakapowasili kuchukua nafasi ya majeshi hayo na kuzuwia wanamgambo wa Hizbollah kupata tena silaha.