1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Blair na Olmert wajadili suala la Palestina

5 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSY

Tony Blair,alie mjumbe maalum wa kundi la pande nne kutafuta suluhisho la amani katika Mashariki ya Kati,amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert,kujadili suala la kuunda taifa la Palestina.Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Israel,mkutano uliofanywa mjini Jerusalem umehusika na vipi Blair atasaidia kuimarisha taasisi za Kipalestina pamoja na uchumi na vikosi vya usalama,ili kuweza kupata msingi wa kuunda taifa huru la Palestina.