1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Israel kubabidhi mji mwengine kwa Palestina

20 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFV6

Israel inapanga kukabidhi udhibiti wa mamlaka ya mji wa Ukingo wa Magharibi wa Tulkarm kwa Mamlaka ya Palestina hapo kesho.

Waziri wa Ulinzi Shaul Mofaz amesema maafisa wa Israel na Palestina watakutana baadae leo hii kukamilisha mipango ya kuukabidhi mji huo ambao ni wa pili kati ya miji mitano inayopangwa kukabidhiwa kwa Wapalestina.

Tangazo hilo linakuja wakati kumezuka machafuko ya umwagaji damu huko Ukingo wa Magharibi ambapo Wapalestina wenye silaha waliwafyatulia risasi wanajeshi wa Israel katika kambi ya wakimbizi karibu na Ramallah na kuwajeruhi wanne.

Nao wanajeshi wa Israel wamemjeruhi Mpalestina mmoja katika kizuizi cha barabara karibu na Bethlehem.