1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Israel yakataa masharti ya Palestina

2 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCe0
Moshi wafuka katika kambi ya wakimbizi ya Nahr al_Bared
Moshi wafuka katika kambi ya wakimbizi ya Nahr al_BaredPicha: AP

Israel imekataa masharti ya Palestina ya kuwaachilia wafungwa takriban 1,500 wa kipalestina wanaozuiliwa katika jela za Israel. Palestina imeweka masharti hayo ili mwanajeshi wa Israel, koplo Gilad Shalit, anayezuiliwa na wanamgambo wa kipalestina aachiliwe huru.

Israel imesema mazungumzo kuhusu kubadilishana wafungwa yanayodhaminiwa na Misri kwa sasa yamekwama. Hata hivyo imesema italegeza sheria katika baadhi ya vituo vya ukaguzi kwenye eneo la ukingo wa magharibi wa mto Jordan kufuatia hatua ya waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, kuahidi kuboresha hali ya kibinadamu ya wapalestina mnamo mwezi Disemba mwaka jana.