JERUSALEM :Israel yashikilia kutoshirikiana na Palestina
19 Machi 2007Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert anatoa wito kwa mataifa tajiri Ulimwenguni kuendelea kusitisha misaada kwa Mamlaka ya Palestina hata baada ya kuundwa kwa serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa.
Kulingana na Waziri Mkuu Olmert serikali mpya ya Palestina haijatimiza matakwa ya jamii ya kimataifa ya kusitisha vita na kutambua taifa la Israel.
Serikali mpya ya Palestina inawashirikisha wafuasi wa vyama vya Hamas na Fatah kinachoongozwa na Rais Mahmood Abbas.
Wakati huohuo ubalozi mdogo wa Marekani mjini Jerusalem unasema kuwa hautaacha kuwasiliana na wabunge katika serikali mpya wasiokuwa katika chama cha Hamas.
Raia wa Palestina walikuwa na imani kuwa ushirikiano kati ya vyama vya Hamas na Fatah huenda ukaondoa vikwazo vya fedha ilivyowekewa na mataifa ya magharibi na kutoa wito kwa serikali mpya kupewa nafasi.